Alhamisi 27 Novemba 2025 - 00:23
Ataba Tukufu ya Imamu Hussein (a.s) Yajenga Makazi ya Bure kwa Watu Wenye Uhitaji

Hawza/ Atabat Takatifu ya Imamu Hussein (a.s) imetangaza kukamilika kwa mfano wa kipekee wa makazi kwa watu wenye uhitaji kama awamu ya kwanza kwa ngazi ya Iraq, unaojumuisha nyumba 3000 katika mkoa wa Basra.

Kwa mujibu wa taarifa ya Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Ataba Takatifu ya Imam Husseini imeripoti kukamilika kwa mfano huu wa kipekee wa makazi kwa watu wenye uhitaji kama awamu ya kwanza kwa ngazi ya Iraq, unaojumuisha nyumba 3000 katika mkoa wa Basra.

Ataba Takatifu ya Husseini imetangaza kuwa ujenzi wa nyumba 3000 katika mji wa “Al-Thaqalayn” kwa ajili ya watu wenye mahitaji umehitimishwa kama awamu ya kwanza katika mkoa wa Basra.

Mhandisi Safwan Ahmad Al-Safi, msimamizi wa kitengo cha miradi ya kusini katika idara ya miradi ya uhandisi na ufundi inayohusiana na Ataba Takatifu ya Husseini, alisema: Mradi unaotekelezwa na Atabatu Takatifu ya Imam Husseini katika mkoa wa Basra umejengwa juu ya eneo linalokadiriwa kuwa karibu mita za mraba 500,000, na unajumuisha nyumba 3000.

Akaeleza: Ataba Takatifu ya Imam Husseini imekamilisha operesheni ya ujenzi wa awamu ya kwanza ya mradi huo, yaani ujenzi wa nyumba 250 katika mkusanyiko wa makazi ya Al-Thaqalayn kwa watu wenye uhitaji katika mkoa wa Basra, na nyumba hizo ziko tayari kukabidhiwa kwa familia maskini zenye mahitaji na familia za mashahidi.

Al-Safi aliongeza: Awamu ya pili itajumuisha ujenzi wa nyumba 750 pamoja na shule, vituo viwili vya afya, msikiti mkubwa, kituo cha manunuzi, maeneo ya kijani, viwanja vya michezo ya watoto, na viwanja kadhaa vya mpira wa miguu.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha